Saturday, July 28, 2012
SHETTAH THE DON
WAKATI baadhi ya vijana wa dini ya kiisilamu waliokuwa single sasa wengi wameshavuta watoto ndani kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa upande wake msanii anayefanya vizuri kwenye soko la muziki wa kizazi kipya kwa sasa Shetta, amedai kuwa hakufunga ndoa kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Shetta anaamini kuwa wapo baadhi ya vijana wameamua kuvuta jiko kwa lengo la mwezi wa Ramadhani, ili waweze kutulia ndani lakini hilo haoni kama ni zuri kwani wengi wanaweza kuachana na wake zao baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.
Hata hivyo kwa upande wa ndoa yake anadai kuwa maisha yanaenda vizuri kwani hali imekuwa tofauti na pale alipokuwa single, ambapo sasa anafurahia maisha ambayo hakuwahi kuishi tangu azaliwe.
“Maisha matamu sana ukiwa na mke unayempenda naye anakupenda ndani ya ndoa yangu mambo ni safi yani najisikia raha sana, ingawa wapo baadhi ya vijana wenzangu ndani ya ndoa zao ni matatizo kila
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment