Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas atahudhuria sherehe za kuapishwa rasmi rais mpya wa Brazil Dilma Rousseff jumamosi ijayo. Lakini kabla ya hapo Bwana Mahmoud Abbas leo anatarajiwa kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa ubalozi wa Palestina mjini Brasilia. Mapema mwezi huu Brazil iliitambua Palestina kuwa nchi huru katika mipaka ya kabla ya mwaka wa 1967.
Brazili ni miongoni mwa nchi chache ambazo hivi karibuni zimeitambua Palestina kuwa nchi huru.
Mazungumzo baina ya Israel na wapalestina yanayofanyika kwa upatanishi wa Marekani, yalisambaratika mapema mwaka huu baada ya Israel kukataa kusimamisha mpango wa ujenzi wa makaazi zaidi ya walowezi wa kiyahudi kwenye maeneo ya wapalestina.
No comments:
Post a Comment