Friday, December 31, 2010
Happy New Year
Wafanyakazi wa Sea Cliff Resort and Spa ya Zanzibar wamewalalamikia ma boss wao kwa kuwagandisha.
Mahmoud Abbas aenda Brazil
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas atahudhuria sherehe za kuapishwa rasmi rais mpya wa Brazil Dilma Rousseff jumamosi ijayo. Lakini kabla ya hapo Bwana Mahmoud Abbas leo anatarajiwa kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa ubalozi wa Palestina mjini Brasilia. Mapema mwezi huu Brazil iliitambua Palestina kuwa nchi huru katika mipaka ya kabla ya mwaka wa 1967.
Brazili ni miongoni mwa nchi chache ambazo hivi karibuni zimeitambua Palestina kuwa nchi huru.
Mazungumzo baina ya Israel na wapalestina yanayofanyika kwa upatanishi wa Marekani, yalisambaratika mapema mwaka huu baada ya Israel kukataa kusimamisha mpango wa ujenzi wa makaazi zaidi ya walowezi wa kiyahudi kwenye maeneo ya wapalestina.
Kamanda wa polisi wa Borno
Kamanda wa polisi wa Borno
Mapigano kati ya kundi hilo na polisi yamesababisha vifo vya mamia ya watu tangu mwaka jana.
Kundi la Boko Haram lilidai kuhusika na mashambulio ya mabomu ya siku ya kuamkia Krismasi katika jiji la Jos ambayo yalisababisha vifo vya watu wapatao 80.
Mkuu wa polisi kamishna Mohamed Abubakar Jinjiri ameiambia BBC Idhaa ya Kihausa kuwa watu watano wameuawa katika mashambulio hayo. Amesema miongoni mwa waliokamatwa ni mtu anayeshukiwa kuwa mdhamini wa Boko Haram, ambaye alikuwa na vifaa vya kutengenezea bomu nyumbani kwake.
Wakati huohuo msemaji wa jeshi, Luteni Abubakar Abdullahi ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu wanane wameuawa
Subscribe to:
Posts (Atom)